Text Size
Tanzania: (Ki)Swahili

Karibu

flag tanzania

MAISHA YAKO HAITAKUWA JINSI ULIVYO
NA: Mwinjilisti Sieberen Voordewind
RAFIKI MPENDWA: HITAJI LAKO NI LIPI?
KUSHUSHWA MOYO: UOGA, UCHUNGU, HUZUNI, MATESO, KUFINYILIWA, KUHUKUMIKA MOYONI NA KUKOSA UTULIVU KATIKA MAISHA YAKO?
JE WEWE NI MGONJWA? NIKO NA UJUMBE MZURI KWAKO.
NIKO NA BIBILIA KATIKA MKONO, KUNA NGUVU ZAIDI YA UWEZO WOWOTE WA ULIMWENGU HUU. NI NENO LA MUNGU: BIBILIA
Bibilia inasema: 'ukaniite siku ya mateso, nitakuokoa na wewee utanitukuza (Zaburi 50:15)
Haya siyo mafundisho ya kanisa la ubatizo, au Kikatoliki, Pentecote, au mafundisho ya kanisa. Lakini ni agano la ahadi kutoka kwa Mungu aishie milele.
Mungu akasema: "Mimi ndimi Bwana nikuponyae" (Kutoka 15:26) Nguvu za Mungu ziko tayari kuponya wewe! Pia Nguvu za Mungu ziko tayari kuwasaidia siku ya leo! Ndio Bibilia inasema, Mwizi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu, mimi (Yesu mwana wa Mungu) nilikuja ili wewe (nyinyi) na muwe na uzima, kasha wawe nao tele".
(Yohana 10:10)
Hii ni habari njema: nawaletea habari njema rafiki, bibilia inasema, "roho ya Bwana Mungu I juu yangu, kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubirie wanyenyekevu habari njema, amenituma ili kuwaokoa walovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. (Isaya 61:1)
Habari njema ni hii: "akusamehe maovu yako yote. Akuponye magonjwa yako yote" (Zaburi 103:3)
Habari njema ni hii: Yesu atakusaidia na iwapo utafanya yale bibilia inasema: soma bibilia: amini bibilia na ufanye yale ambayo inasema.
NENDA KWA YESU NA MAHITAJI YAKO YOTE, NA MAISHA YAKO HAITABAKI JINSI ILIVYO!
Nasema: maisha yako haitabaki jinsi ilivyo" Hallo! Nenda kwa Yesu na Yesu! Nenda na mahitaji, uchungu na dhambi zako. Yesu ndie ukweli na uzima. NDIO YESU ANATAKA KUKUTENDEA MIUJIZA.
Miujiza ni jambo ambalo haliwezi kutendeka kwa uwezo wa mwanadamu. Miujiza sio kazi ya waume au wanawake. Huu ni wakati wako wa miujiza!
Ni wakati wa kufunzwa na Yesu ili upokeee muujiza waki.
Halluluhya! Je uko tayari kuchukuwa muujiza uliyo mkuu?
TAFADHALI OMBA NAMI,
"Bwana Yesu nisamehe dhambi zangu, nimehuzunika kwa ajili ya dhambi zangu, nisafishe na damu ya Yesu Kristo, fungua moyo wangu na ukaingie ndani. Nisafishe na inifanye upya na damu ya Yesu kristo na unikubali kama mwanao. Nimekubali wewe huwa mwokozi na mkombozi wa maisha yangu. Asante Bwana kwa maana ulinifia pale msalabani, kwa niaba ya dhambi zangu. Amina!
Amani! "Bibilia inasema, "damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafishe dhambi yote.." (1 Yohana 1:7b)
Na kwa sasa maisha yako hayatakuwa jinsi ilivyo ikiwa utatembea na Yesu (1 Yohana 1: 5-2, 14/Matendo ya mitume 26:18)
Kwa hivyo na kuombea upako wa kawaida na maombi.
Toa macho yako ya kawaida juu ya hali na utarajie muujiza kutoka kwa nguvu za Mungu. Nguvu za roho mtakatifu katika jina la Yesu.
Ikiwa mahitaji yako namna gani usisahau hakuna jambo gumu kwa wale wanao mwamini Yesu Kristo, Mwana wa Mungu aishie,
Je, ukotayari rafiki yangu weak mkono wako juu ya huu ujumbe naomba, "Mungu wangu katika jina la Yesu Kristo, ninakuja kwako na huyu mume, mke, kijana na msichana ambae anahitaji, ninakusihi ukamguse mtu huyu kwa nguvu zako takatifu katika jina la Yesu. Bwana mponye Mtu huyu kwa asilimia moja. (100%)
Mponye kutoka juu kichwani hadi miguuni, tunaomba shida zake zote Bwana ukawee kufanya miujiza. Ewe rafiki yangu pokea uponyaji katika Jina la Yesu. Pokea ukombizi kutokana na shida zako zote katika jina la Yesu na ukapokee nguvu za Roho Mtakatifu na upako sasa katika jina la Yesu nakuweka huru, Amen"
"bali alijeruhiwa (Yesu) kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu. Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake na kwa kupigwa kwake sisis tumepona" (Isaya 53:5)
Usisahau Mungu ni mkuu kila wakati hata kuliko mahitaji yako!
Mungu anakupenda.
"basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji (Waebrania 4:16)

Maisha yako haitabaki jinsi yalivyo
Tuma ombi l;a maombi kwa: Dit e-mailadres wordt beveiligd tegen spambots. JavaScript dient ingeschakeld te zijn om het te bekijken. Dit email adres wordt beschermd tegen spam bots, u heeft een Javascript-enabled browser nodig om berichten te kunnen lezen

Swahili translation: Alfred Musunga
TRANSLATION OF YOUR LIFE WILL NEVER BE THE SAME*************
PERNI NANI MSHAURI WAKO?
Kipindi cha kutafakari na maombi kupitia kwa redio
na mwinjilisti sieberen voordewind

Ewe msikilizaji wa hiki kipindi ningependa kuongea na wewe juu ya ujumbe huu: Ni nani mshauri wako? Tafadhali fungua moyo wako kwa ajili ya neno la Mungu anayeishi wakati unaponisikiliza ili uweze kupokea baraka tele tele.
Bibilia inasema yeyote anayemtumainia Yesu hataaibika kamwe Warumi 9:33. Shida yako inaweza kuwa nini? Tunasoma katika Bibilia kuhusu mtu aliyeingia katika shida kubwa jina lake Yehoshafati. Bibilia inaeleza yafwatayo katika kitabu cha 2 mambo ya nyakati 20:2 na 3a wakaja watu wakamwambia Yehoshafati wakisema wanakuja Jamii kubwa juu yako watokao shamu_ _ _ _
Yehoshafati akaogopa_ _ (Bibilia ya Dutchi, NBG. 1951)
Pengine umekuwa kama Yehoshafati na umekuwa katika mateso na kuishi katika uoga. Uoga wa siku za usoni au kuwa na upweke, kufa au kufilisika au umeogopa kuwa hautaondoka katika ugumu huu. Chochote unachohitaji au kuogopa, swali langu ni hili: "Ni nani mshauri wako?" Ndio unamwendea nani ukiwa na shida na uoga fanya jinsi Yehoshafati alivyofanya! Bibilia inasema "Yehoshafati akaogopa akauelekeza uso wake amtafute bwana".
Bibilia ya Dutch NBG 1951) Aliambiwa kufuata Mungu na mahitaji yake Mungu anayesikia maombi na kujibu yote kulingana na mapenzi yake kwa wakati wake. Bibilia inasema katika msitari wa 3: "Yehoshafati anatangaza mbiu ya watu kufunga katika Yuda yeyote.
Bwana asifiwe Yehoshafati akatafuta kinga yake, siyo kwa mwanadamu lakini kwa Mungu. Hali yake haikuwa ya matumaini ndio kwa sababu akaomba "maana hatuna uwezo juu ya jamii kubwa hii" (msitari wa 12) Labda unahisi hauwezi kukumbana na hali hii ambayo umo ndani.Hali yake ni ya kibinadamu haina tumaini.Yehoshafati akasema: "hatujui la kufanya,"Na hata haujui lakufanya.Lakini ni nani mshauri wako?Je unamwendea nani kwa ajili ya usaidizi?Yehoshafati alimrudia Mungu na kuomba "lakini macho yako iko juu yako hakuona kuasi kwa watu,lakini alimuangalia Mungu kwa imani ambayo kila jambo linawezekana.Alivyoendelea kuomba Biblia inasema(mstari wa 14) " Roho wa Bwana akamjia Yezieli akasema sikieni Yuda wote nanyi mkaao Yerusalemu na wewe mfalme Yehoshafati Bwana asema hivi,msiogope wala msifadhaike kwa ajili ya jeshi kubwa hili,kwani vita si yenu bali ni ya Mungu.Kesho shukeni juu yao ,tazameni wanakweya kwa kupandia sisi," nanyi mtawapata penye mwisho wa bonde,mbele ya jangwa la Yerudi.Hamtahitaji kupigana vita, jipangeni, simameni mkaone wokovu wa Bwana uliyo pamoja nanyi enyi Yuda na Yerusalemu ,msiogope ,wala msifadhaiki kesho tokeni juu yao,kwa kuwa Bwana yu pamoja nanyi.
Wakati walipokuwa katika maombi na wenzao roho wa Bwana akaja na jawabu .Je ni ya ajabu namna gani?Na kwa Rehema zetu tuko na vitabu vilivyotiwa pumzi na roho mtakatifu ambaye kila jawabu limeandikwa ndani .Kitabu hiki kinaitwa Biblia.
Biblia inasema hivi, niite nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa ,magumu usiyoyajua.Tazama nitakuletea afya na kupona ,nami nitawaponya" (Yeremia 33:3-6)
Ukimkubali Mungu aliyehai kuwa mshauri katika maisha yako atakunenea kupitia kwa maombi.Biblia au kwa njia nyingine,usaidizi wake ni wa kipekee ushauri wake ni wa ajabu fanya jinsi Yehoshafati alivyofanya uamuzi wa kutafuta msaada kutoka kwa ushauri wa Mungu.
Jinsi ilivyo kuwa na Yehoshafati Bwana atasikia maombi yako na katika wakati wake atakujibu.
Baada ya Mungu kujibu Yehoshafati "Yehoshafati akainama kichwa,kifulifuli,wakaanguka mbele za Bwana Yuda wote na wakaao Yerusalem,wakimsujudia Bwana (2 mambo ya nyakati 20:18)
Hata baada ya shida kusuluhishwa aliamini ushauri wa Mungu na akainama na kumuabudu Mungu .Wakati Mungu anaponena nasi kupitia kwa maombi na Biblia tunaposema hatuoni jawabu kwa shida zetu kwa macho ya mwanadamu .Jambo la kuanza yafaa tuamini jawabu na ushauri wa Mungu kabla hatujaona, Yesu akasema katika Mariko 11:24 "kwa sababu hiyo nawaambia,yoyote myaombayo mkasali,aminini ,ya kwamba mnayapokea ,nayo yatakuwa yenu.
Amini ya kwamba maombi yako yamesikika kwa Mungu kabla ya kuona mabadiliko .Anza kumshukuru Mungu kwa ajili ya muujiza .Kama vile Yehoshafati Bwana Mungu atajibu maombi yako kulingana na mapenzi yake.Kwa wakati wa Mungu utatoka ndani ya shida zako na utakuwa tayari tutembee kwa amani na furaha kama mfalme Yehoshafti .Haya tunaweza kusoma katika neno la Mungu.
"Kisha wakarudi ,kila mtu wa Yuda na Yerusalem kwa furaha ,kwa kuwa Bwana amewafurahisha juu ya adui zao.Wakafika Yerusalem wenye vinanda ,vinubi na mapanda kwenda nyumbani kwa Bwana .Ikawa hofu ya Mungu juu ya falme zote za nchi ,waliposikia ya kuwa Bwana amepigana juu ya adui za Israeli Basi ukatulia ufalme wake Yehoshafati ,kwa sababu Mungu wake alimstarehesha pande zote."(Mambo ya Nyakati 20:27-30)
Bwana asifiwe kwa yote ambayo Mungu alimfanyia Yehoshafati nakumtendea k katika jina la Yesu kristo wa Nazareti ambaye amekuja duniani kutakaza wenye dhambi.Popote ulipo wakati huu, katika chumba cha kuishi ,jela ,na dani ya gari,au popote .Enda kwa imani katika kiti cha enzi cha Mungu.
"Ewe Mungu na baba yetu ,katika jina la ajabu la Yesu Kristo nimekuja kwako na wote ambao wako na hitaji na wananisikia kupitia kwa Radio.Hatuitaji kuwa na shauku lakini tuamini kuwa wewe ni mkuu katika taabu zetu kwa hivyo nakuuliza .Nguvu zako za wokovu ,ukombozi ,uhuru na uwezo wa uponyaji unatoka kwako wakati huu.ponya wangojwa na kuwakomboa kutokana na uchungu ,waweke uhuru kutoka kwa ufungwa,hofu.Ondoa kila shida yote ya kifedha na ukapeana mahitaji yao .Ewe Bwana onekana kwa msikilizaji huyu kwa nguvu na upako ili maisha yao baada ya hiki kipindi isikuwe jinsi ilivyo.Nakushukuru kupitia kwa rehema zako utasikia maombi haya na kuyajibu .Nina sifu na kutukuza jina lako takatifu.
Rafiki yangu mpendwa pokea uponyaji ,uhuru suluhisho na upokee upako wa roho wa Mungu katika jina la yesu .Ninaamini na kushukuru kwa haya na kutosahau ni nani mshauri wako?
Nakutakia Baraka za Mungu katika jina tukufu la Yesu Kristo lililo juu ya majina yote .Amina.

Ujumbe huu umetafsiriwa na mchungaji Alfred Musungu.
TRANSLATION OF WHO IS YOUR ADVISOR IN KISWAHILHILI*************
LINK/Kiungo:

1) Kenya Assemblies of God:
http://www.kagburuburu.org/index.php?option=com_frontpage&Itemid=1

2) REVIVAL EXPLOSION CENTER INTERNATIONAL MINISTRIES (R.E.C.I.M)
Karibu katika ibada zetu: kila jumapili na mchungaji ALFRED MUSUNGU.
Kwanzia 9.00am – 12.45pm.
KUHUSU SISI /KANISA
Hili ni kanisa la kiroho ambalo linaenenda katika uwezo wa roho mtakatifu kama zile nguvu ambazo zilionekana wakati wa siku ya pentecote.( Matendo ya mitume 2) Waumini waliweka misingi yao katika maombi, ushirika na kuumeka mkate katika mafudisho ya mitume ( matendo ya mitume 2. 42-46). Kwa hivyo kanisa hili ni la kiroho na maono ya kutumikia mungu.
MAHALI TUNAPATIKANA
Kanisa hili linapatikana katika nchi ya Kenya, Kakamega (sehemu ya magharibi ya Kenya)
MAONO YA KANISA
KUANDAA WATU WA MUNGU KWA AJILI YA KURUDI KWA YESU CHRISTO. " Itengenezeni njia ya Bwana yanyosheni mapito yake. (Luka 3.4)" Maono haya ni kuwasaindia wakristo kuelewa kurudi kwa Yesu Kristo na kuja kunyakua kanisa. Anarudi kwa ajili ya kanisa lililo takatifu, kanisa lisilo na lawama, kanisa ambalo limeandaliwa kikamilifu kwa ajili ya Yesu Kristo. " Kwa hivyo ninyi nanyi jiwekeni tayari kwa kuwa katika saa msiyodhani mwana wa Mungu yuaja ( Mathayo 24:44)" Kwa hivyo inatupasa kuishi katika dunia hii tukijua kwamba siku moja Yesu Kristo yuaja mara ya pili kunyakua kanisa. Katika haya maono yatufaa kuelewa ya kwamba tunastahili kujiadaa kumtumikia Bwana katika uaminifu na kuwa tayari kwa kazi ya huduma. Kwa maana sisi ni vyombo vya kutumiwa na Mungu kuandaa kanisa ili liwe tayari kwa kurudi kwa Yesu Kristo.
WAJIBU
Ni kufikia ulimwengu na injili ya Yesu Kristo (Mathayo 24:14).
LENGO/JUKUMU.
Kanisa ni la kimutume na mwito wa kuanzisha makanisa mengine katika ulimwengu wote. Yafaa tuhubiri yesu Kristo aliyesulubishwa na kufufuka kwa ulimwengu wote na kutangaza ujumbe wa tomba, urejesho na utakatifu kwa watu wote wanapojiandaa kwa kurudi kwa yesu Kristo. Kanisa linafaa kuwafanya waumini kuwa wanafunzi ( na kuwanjenga katika huduma zao na gharama za roho mtakatifu) ili waweze kuwa tayari kwa ajili ya kazi ya bwana kupitia kwa mafudisho na mahubili. Kuinua kikudi cha mitume na manabii kupitia kwa mafudisho diposa waweze kuhubiri injili ya Yesu Kristo kwa mataifa yote. Kusidia wale ambao wana mahitaji kama watoto watima, wanjane, waliofiwa na kuombea wagonjwa nyumbani na hospitalini. Kushuhudia Kristo na kuanzisha ushirika wa Nyumbani katika vijiji kama moja wapo ya mpangilio wa kanisa. Kufanya uinjiristi na umishonari katika mataifa. Kuombea taifa na wale ambao hawanja okoka katika jamii na kufikiwa na neon la Mungu. Kuanazisha shule na makao ya watoto mayatima na hospitali katika jamii.
MAMBO AMBAYO TUNAAMINI.
Tunaamini kuwa Bibilia ni neon la Mungu ambalo limetiwa pumzi na Mungu mwenyewe na halina dosari yoyote katika mandishi yake na lina mamlaka katika mambo ya imani ( 2 Timotheo 3:15 – 17) Kuna Mungu mmoja anayeishi milele katika utatu: Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu. ( Mathayo 28:19 ) Tunaamini ya kwamba kila mwanadamu ni mwenye dhambi na amepungukiwa na utukufu wa Mungu, kwa hivyo anahitaji kuzaliwa mara ya pili kupitia kwa roho mtakatifu na anahitaji ukombozi na wokovu wa Yesu Kristo kwa neema katika imani ( Yohana 3:5- 8, Waefeso 1:7, 2:8) Roho Mtakatifu anakaa dani ya muumini na humfanya kuishi maisha matakatifu. Tuna amini katika ubatiso wa roho Mtakatifu katika moto na kujazwa na roho Mtakatifu katika maisha ya muumini. Kuna kufufuliwa kwa wale ambao wameokoka na walio potea. Tunaamini katika ubatizo wa maji mengi ambao tunatoa ushahidi ya kwamba muumini amekufa amoja na Kristo na pia amefufuliwa na Kristo ili akaenende katika maisha mapya. Na kadhalika.
HABARI ZA KIBINAFSI ALFRED MUSUNGU;
Mimi nilizaliwa mwaka 1975 katika kijiji cha Ebunangwe, wilaya ya vihiga katika nchi ya Kenya ,Afrika mashariki. Nilipokea Yesu kristo kama mwokosi wa maisha yangu mwaka wa1996 katika kanisa la nyumbani.Nimekuwa mchungaji msaidizi katika la nyumbani kwa miaka (.8) ,hadi wakati ambapo bwana aliniita ili nifanye kazi yake ya huduma.Ksha akanipa maono ya kanisa hili REVIVAL EXPLOSION CENTER INTERNATIONAL MINISTRY.Ambapo mimi ndiye mchungaji mkuu pamoja na mke wangu. Kupitia Kwa maombi tunajipa moyo ya kwamba tunawekufikia ulimwengu na injili ya Yesu Kristo (mathayo24:14). Bwana awabariki: Amina.
REVIVAL EXPLOSION CENTER INTERNATIONAL MINISTRY ALFRED A.MUSUNGU.
SANDUKU LA POSTA; 1973 KODI YASANDUKU; (50100) KAKAMEGA KENYA AFRIKA MASHARIKI. NAMBARI YA SIMU; +254-726-499-728 ANUANI PEPE; Dit e-mailadres wordt beveiligd tegen spambots. JavaScript dient ingeschakeld te zijn om het te bekijken. Dit email adres wordt beschermd tegen spam bots, u heeft een Javascript-enabled browser nodig om berichten te kunnen lezen
AKAUNTI YA BENKI; 111498683 KENYA COMMERCIAL BANK, TAWI LA KAKAMEGA. NIMEOA MKE NIKO NA WATOTO MIMI NIMZALIWA WA KENYA KAZI; MCHUNGAJI WA KANISA*************

MUNGU ANIONA KUWA MTU WA AJABU
Kutafakari kupitia kwa redio na mwinjilisti Sieberen Voordewind

Ewe mpendwa msikilizaji, unahisi ya kwamba wewe ni kitu bure? Je kulingana na watu wengine wewe ni 'sehemu ya uchafu?' Pengine Watu wengine wamekushusha na kudharau kwa sababu wanakuona kuwa mtu asiyependeza na asiye na uhusiano na hata hauwezi kudhaminiwa. Pengine haujapendwa na watu wa jamii yako, marafiki au kukubalika na watu wengine. Maongezi yao ni ya kushusha moyo na hata kulingana nao wanakuona kuwa hautawahi faulu au fanikiwa katika maisha yako. Ahaa unahisi uchungu na huzuni katika moyo wako.
Lakini hakuna mtu anayeona machozi unahizi kuwa na uoga.Je utafanya nini?Rafiki yangu au mchumba wangu ,haujakosea kwa kusikiliza ujumbe huu ambao una uwezo .Nina habari ya ajabu kwako .Watu ambao nimetaja hapa wameshikilia kioo kibaya mbele yako.Kwa mafano umewahi kuwa katika chumba kilicho na aina zote za vioo vya kuchekelea ambavyo vimsimesimama kwa ukuta.
Kabla ya kioo kingine,unatazama kioo kingine baada ya kingine ambacho ni mbaya sana. Kila kioo kina sura yako;ijapokuwa tulikuwa na vioo vingi ambavyo vilikuwa na umbo lako. Je,unajua ninamaanisha nini?Hatukuwa na jambo baya kuhusu wewe lakini vioo.Vioo hivi viliharibiwa na sio wewe.
Ni vibaya watu kuonyesha "kioo kibaya"kupitia kwa maneno na vitendo vyao.Kwa "kuonyesha kioo"kibaya uliamini maneno yao.Wakasema :"wewe ni takataka. Jambo la kustaajabisha ni uliamini kwamba wewe ni "takataka"Usiamini uongo wa watu wengine. Mungu aishiye anakuona kuwa mtu wa ajabu na wa dhamana sana.
Pengine unasema "Mimi ni mwenye dhambi na Mungu ananichukia". "La hasha Mungu anachukia dhambi;lakini sio mwenye dhambi kwa maana Mungu anakupenda kikamilifu sana.Ndio maana jinsi hii alimtoa mwanawe pekee ili kufia dhambi zako.
Soma katika bibilia Yohana 3:16.Mungu anakupenda na anataka ukaweze kupata uzima wa milele .Ni bure: na---hakuumba kutoka kwa tumbili.Bibilia inasema: "Maana wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu,uliunga tumbo mwa mama yangu.Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha (zaburi 139:13-14).Ni Mungu aliyekuumba pengine kwa watu wengine hawahesabu, lakini Mungu anahesabu.Mwanawe Yesu Kristo anataka kuwa rafiki yake.
Je utakuaje katika uhusiano na yeye?Fanya hivi kwa kupiga magoti na kumuuliza Yesu kingia katika moyo wako na kufanya upya.Mwambie uchungu na huzuni wako.Soma Biblia haswa kitabu cha injili ya Yohana.Amini Biblia na utende jinsi inavyoeleza.Biblia ndio kioo cha maana. Mungu anakuona kuwa mtu wa ajabu.
Mungu akaumba mtu kwa mfano wake kwa mfano wa Mungu,aliumba mwanaume na mwanamke aliumba .........Mungu aliwabariki.(Mwanzo 1:27) ninawatakieni baraka za Mungu amina.

Ujumbe huu umetafsiriwa na mchungaji Alfred Musungu
Translation of: God finds you unique*************
POKEA ROHO MTAKATIFU
kutafakari na maombi kupitia kwa Redio na mwinjilisti Sieberen Voordewind

Ewe msikilizaji fungua moyo wako kwa ajili ya neon la Mungu aishiye kwa sababu niko na ujumbe kwa ajili yako kuhusu Roho wa Mungu na uweza wake.Je unatamani uwepo wa Mungu katika maisha yako?Je unatamani uweza au nguvu za Mungu na utakaso?Ungependa kuambia watu kuhusu Mungu lakini unahisi kuwa hauna ujasiri?Je unatamani kutulizwa na mungu kutoka kwa huzuni wako?ahaa,niko na ujumbe mkuu kwako.Mungu aishie milele yuko tayari kukujaza na Roho mtakatifu na nguvu zake.
Baada ya Yesu Kristo kupaa juu mbinguni Bwana Mungu alituma Roho Mtakatifu kukaa ndani ya wafasi wa Yesu.
Katika Biblia tunasoma kuhusu mtume Paulo alipowauliza wafuasi wa Yesu Kristo katika kitabu cha Waefeso:Je mlipokea Roho mtakatifu mlipoamini?[matendo ya mitume 19] Je unafikiri waumini walijibu nini?Wakajibu:"La hasha hatujawahi sikia kwamba kuna roho mtakatifu."Alikuwa anashughulika na wauamini .Ndugu Paulo alielewa ya kwamba walikuwa wamepatiswa katika maji.Kwa hivyo akawauliza: "Je ni ubatiso gani mliopokea?' Ubatiso wa Yohana." Wakajibu.
Ndipo wakabatiswa tena kimuijiza katika jina la Bwana Yesu.Lakini haya yote haikutosha kwa sababu hawa waumini waaminifu walikuwa hawajajazwa na Roho mtakatifu!hadi Paulo alipowawekelea mkono na Roho mtakatifu akakuja juu yao na wakanena katika ndimi na kutabiri.
Katika nyakati hizi kuna wapendwa ambao ni wafuasi wa Bwana Yesu ambao hawajajazwa na Roho mtakatifu.Wanahudhuria kanisa kwa uaminifu kila wiki.Pia wanaweza kuwa sehemu ya wale wanaofanya uinjilisti.Wanaongea kuhusu Yesu na Roho mtakatifu .Lakini wanakosa uhusiano wa karibu wa Roho mtakatifu katika maisha yao kuongea,kuimba au kusoma kuhusu Roho Mtakatifu sio sawa kujuwa yeye.Iwapo ungependa kujua mtu huyu ni vyema kuwasiliana na yeye .Muruhusu nyumbani mwako;nena na yeye msindikize popote anapoenda.Hii ni sawa katika ulimwengu wa kiroho.Kwa kujua Roho mtakitafu ni lazima uwasiliane na yeye.Ni lazima umuruhusu katika maisha yako.Unene na yeye.Na anaponena na wewe,ni lazima uwe tayari kwa kusikiliza .Na akikuonyesha njia,lazima ufuate hiyo njia pamoja na yeye .Hivi ndivyo unavyo kuja kumtambua.Ni jambo la kustaajabisha katika maisha yetu.Sio tu ndini lakini ni maisha yako na Roho mtakatifu .Na hiyo inawezekana, Bwana Yesu angependa kupea Roho mtakatifu .Lakini hakuna gharama yoyote ya kulipia hata ya kifedha.Katika Bibilia tunasoma kuhusu mtu mmoja ambaye alifikiria kuwa ataweza kununua Roho mtakatifu [Matendo ya Mitume 8] wakati Simeoni alipoona Roho akipean wa wakati wa Mitume walipowawekelea mikono.ilibidi apeane pesa na kusema ,"Nipe pia huu uwezo ili yeyote nitakayewekelea mkono akaweze kupokea Roho mtakatifu."Uangamie na pesa zako maana ulifikiria kwamba utaweza kununua kipawa cha Mungu kwa kutumia pesa.
Roho matakatifu hawezi kununuliwa kwa kutumia pesa.Pia Roho mtakatifu hawezi kupatikana kuwa kung'ang'ana.Roho mtakatifu hawezi kupatikana kupitia kwa kujiandikisha kanisani.Roho mtakatifu hatoki kwa mwanadamu,Roho Mtakatifu hatoki Amerika au Afrika.Roho mtakatifu hatoki katika dhehebu la Kipentecote.Roho Mtakatifu anatoka kwa Mungu aishiye,muumba wa mbingu na ardhi !Mungu mkuu anataka kujaza na Roho mtakatifu.Je ni mambo gani ambayo unahitaji kutimiza?
Wakati Bwana Yesu alipokuwa hapo duniani alisema:"mkinipenda mtazishika amri zangu.Nami nitamwomba Baba,naye atawapa msaidizi mwingine ili akae nanyi hata miliele '[Yohana 14:15-16]
Bwana Mungu anataka kujaza na roho mtakatifu iwapo unampenda mwanawe Yesu kristo na kutii yale ambayo anataka ufanye. Je, ungependa kupokea roho mtakatifu? Jambo la kwanza unahitaji yesu kristo katika maisha yako. Mpende na umtii yesu kristo. Popote ulipo ndani ya gari ,jela, gari la moshi. Kuwa tayari kupokea Roho mtakatifu. Jambo la kwanza unahitaji yesu, njoo kwa yesu kila wakati.kama uko tayari sema haya kwa sauti. Bwana yesu, naja kwako jinsi nilivyo, nisingependa kufuata njia zangu lakini zako. Nisamehe dhambi zangu na unitakase kwa damu ya yesu kristo. Iwapo umeomba o mbi hili na maneno iliyo wazi kwa hivyo sasa umefanywa kuwa mwana wa Mungu. Ikiwa unampenda yesu kristo na unataka kumfuata unaweza pia kupokea Roho mtakatifu. Roho mtakatifu atakuonyesha njia na ukweli. Roho mtakatifu atakuhimiza ikiwa una huzuni. Roho mtakatifu atakufanya kuwa mtakatifu. Roho mtakatifu atakusaidia kuomba. Roho mtakatifu atakufunza na kutia nguvu. Bibilia inaeleza katika kitabu cha matendo ya mitume 1:8, " lakini mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu Roho mtakatifu: nanyi mtakuwa mashahidi wangu"
Je Roho mtakatifu anapeana nini? Nguvu. Unahitaji nguvu? Roho mtakatifu anataka kupatia wakati huu. Wakati nilipobatizwa na Roho mtakatifu, nikiwa na miaka kumi na mitano, sikunena katika ndimi tu au nguvu za kiungu ambazo Roho wa Mungu anapeana. Lakini nilihisi nguvu za Roho wa Mungu. Jawabu lake ni nini? Kutokana na hizo nguvu za Mungu, mimi ni shahidi wa yesu kristo mpaka sasa. Jambo la kwanza Roho mtakatifu kisha vitendo na uinjilisti. Bila Roho mtakatifu kila mambo tunayosema na kufanya ni ya nguvu zetu. Bila Roho mtakatifu mimi na wewe tutakuja kwa hekima zetu. Paulo alisema, "nilipokuja kwenu ndugu zangu, sikuja kwa usemi au katika ukuu wa heshima nilipotangaza ushuhuda wa Mungu kwenu. Nilijifanya kutojua lolote nilipokuwa nanyi isipokuwa Yesu kristo ambaye alisulubishwa. Nilikuja kwenu katika udhaifu na uwoga na hofu nyingi. Ujumbe na mahubiri yangu haikuwa ya hekima na maneno ya ushawishi lakini ya kudhibitisha nguvu za Mungu. Ili imani yenu isidumu juu ya hekima ya wanadamu lakini kwa nguvu za mungu" 1 wakorintho 2.
Ndio sikuji kwako na hekima ya wanadamu lakini hekima ya Mungu aishiye. Pia naja kwako kwa udhihirisho wa nguvu za Mungu. Sikuji kwako kwa mafundisho ya wanadamu au kanisa au kuwaletea ndini kwa sababu ndini inasema. Utaokoka kwa kasi yako. Msamaha wa dhambi ni bure. Ubatizo wa Roho mtakatifu ni bure. Kwa usaidizi wa bibilia nimekuletea huu ujumbe ambao Roho mtakatifu ametia ndani yangu.sineni kwa nguvu zangu ila kwa nguvu za mungu.Unahitaji Roho mtakatifu haijalishi kama wewe ni mchungaji,kuhani,mhuduma,mwinjilisti mzee wa kanisa au mchungaji .Unahitaji Roho mtakatifu.Kila mfuasi wa Yesu Kristo alijazwa na Roho mtakatifu.Matendo ya mitume 10.38 inaeleza: "Jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu,"
Yesu Kristo mwana wa Mungu alihitaji Roho mtakatifu.Je ni wingi gani ambao pia wewe unahitaji huyu roho mtakatifu Bwana Yesu alijazwa na Roho mtakatifu kwa hivyo inapasa wafuasi wake kujazwa. Kumtafuta Yesu kunamaanisha kujazwa na Roho mtakatifu.
Kuna watu ambao wamejitolea kufuata Yesu lakini wanapinga Roho mtakatifu.Matendo ya mitume 7:51 tunasoma kuhusu Stefano aliposema na watu ambao walikuwa wamejitolea.Kwa kazi ya Mungu ."Enyi watu walio na shingo ngumu,"mioyo yenu na masikio yenu haijatairiwa muko kama babu zenu:mnapinga Roho mtakatifu kila wakati."
Ni jambo gani lililotendeka baadaye?Bibilia inaeleza Stefano alijawa na Roho Mtakatifu na kulikuwa na watu ambao walijitolea kumpiga hadi akafa.
Ndio hata sasa kuna watu ambao wanapinga Roho mtakatifu.Na sio tu Roho mtakatifu pia hata wakristo ambao wamejazwa na Roho mtakatifu.kuna watu ambao wanapinga ujumbe wa Roho mtakatifu kama huu.Ndio kuna watu ambao ni wakristo lakini wameweza kunirushia mawe ya kiroho na wengi wa wakristo ambao wamejazwa na Roho Mtakatifu.Mkristo anapojazwa na Roho mtakatifu.Kuta kuwa na pingamizi.Lakini kwa nguvu za Mungu hatuhitaji kuogopa uongo au vitina na mashambulizi kutoka kwa watu wengine katika nguvu za Roho mtakatifu pamoja na Yesu Kristo sisi ni zaidi ya washindi.Katika nguvu za Mungu tunasonga mbele kwa nini?Kwa sababu maisha mema ni ya Mungu ,Yesu Kristo na Roho mtakatifu.
Na haya yana husisha wewe.Je,unataka kujazwa.Sasa hivi? Ungependa uzima baada ya hiki kipindi ili ubadilike sasa?
Kama unatamani ubatiso na Roho mtakatifu funguwa moyo wako na nafsi yako wakati huu.Kwa sababu Bibilia inasema katika matendo ya mitume 10:44 "Petero alipokuwa akisema maneno haya Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia ujumbe huu wa Roho uliojaA imani na kuwajenga.Ndio leo ni siku yako.Wakati huu Roho Mtakatifu hajafungiwa wakati au mahali popote.Hakuna mpangilio uliowekwa wa Roho Mtakatifu.Simama kwa imani na utarajia Mungu aishie atakujaza na Roho wake wakati wa hiki
Inua kipindi. mikono yako juu ninapoomba na wewe.
Baba Mungu wetu aliyemkuu ,katika jina la miujiza la Yesu Kristo ninakuja na huyu mpendwa ambaye anatamani kubatizwa kwa Roho Mtakatifu.Hatuihitaji kuwa na shauku lakini tunaamini kwamba wakati huu utamwangalia Roho wako kwa kila moja ambaye anasikiliza ujumbe huu kutoka kwa mtumishi wako.Ndio kwa maana na kuuliza:Tafadhali ruhusu nguvu zako ewe Mungu zikawajaza hawa wote wanaokuamni na wakafikiwe na Roho Mtakatifu.Tunakusifu na kutukuza kwa hayo yote."
Kwa hivyo mpendwa,"Pokea Roho mtakatifu wakati huu.Pokea nguvu za Mungu na utukufu.Pokea sasa katika jina la Yesu Kristo.Simama kwa imani na utembee na Roho mtakatifu.
Nina watakieni baraka za Mungu ,Amina ¡

Ujumbe huu umetafsiriwa na mchungaji
Alfred Musungu.
Translation of: Receive The Holy Spirit

*************
KUINULIWA KUNAPEANWA NA MUNGU
Kutafakari na maombi kupitia kwa redio: na mwinjilisti Sieberen Voordewind

Msikilizaji mpendwa nina furaha kwa sababu unanisikiliza kupitia kwa redio wakati huu na niko na habari njema kwa ajili yako.Mungu aishie milele anataka kuinua! ndio uliumbwa na Mungu kwa ajili ya jukumu Fulani.Hauko dunia hii kwa kutotarajia wala hauko hapa kupoteza maisha yako.Haujawekwa hapa kuzunguka kwa miaka mingi kama mfungwa.
Mungu amekuumba na kipawa unaweza kusoma haya katika kitabu cha Mathayo 25.Sio sehemu ya mpango wako kupoteza kipawa au gharama yako.Unastahili kutumia kipawa chako kwa ajili ya utukufu wa jina la Mungu.Mungu angependa kubariki.
Kwa sababu ya haya, ndio anataka hata kuinua .Biblia inaeleza katika zaburi 75:6-7 "maana siko mashariki wala magharibi wala nyikani itokako hekima.Bali Mungu ndiye ahukumuye humdhili huyu na kumuinua huyu"Ni Mungu ambaye anaweza kuinua ,tarajia kuinuliwa ,kustawi kwako na baraka zako hazitoki kwa binadamu lakini kwa Mungu aishie kupitia kwake mambo yote yanawezekana.
Tunaweza kusoma mfano mzuri kuhusu maisha ya Yusufu kutoka kwa bibilia.Mwanzo 37 inatueleza kwamba Yusufu alikuwa na ndoto.Kuinuliwa kila mara kunaanza na ndoto.Mungu alitaka kumuinua Yusufu .Sasa iwapo angeendelea kukaa nyumbani angekuwa chifu wa kutawala kabila lao.Angekuwa mkubwa wa jamii yao mifugo na hata watumishi wao.Lakini Mungu alikuwa na mpango mzuri kwa ajili ya maisha yake.Kwa kuinuliwa kwake ingelibidi apitie katika chenga moto Fulani katika maisha yake.
Siku moja Yusufu alitupwa katika kisima na ndugu zake.Hali yake katika mtazamo wa kibinadamu haikuwa na tumaini.Tumaini lake la kuinuliwa lilikuwa linadidimia kwa haraka. Mahali pa baya pa kuinuliwa kwake palikuwa ndani ya kile kisima.Lakini Mungu alimuumba Yusufu na mpango fulani.Mungu alitaka kumuinuwa Yusufu.Kwa hivyo wakati ulifika akaondoloewa katika kile kisima.Mungu aliruhusu aishi katika nchi isiyo yake.Yusufu alitoka ndiposa akaweza kuinuliwa.Katika ile nchi geni. Yusufu aliweza kuinuliwa akiwa katika nyumba ya Potifa.Alifanywa kuwa mkurugenzi mkuu.Je haya haikutosheleza?la hasha Mungu alikuwa na mengi katika ghala lake.Lakini ilibidi apitie katika hali ngumu katika maisha yake.Alifungwa jela bila makosa yoyote .Lakini katika jela alipokea kuinuliwa kwingine.Alifanywa mkurungenzi na mshauri akiwa jela.Ilionekana haswa ilikuwa yake.Lakini Mungu alikuwa na zaidi katika ghala lake kwa ajili yake.Wakati watu walipokuwa wamesahahu ,Mungu alimkumbuka.Mungu alimtoa ndani ya jela na kumfanya mkuu!
Mpango wa Mungu kwa ajili ya maisha ya Yusufu haikuwa kuwa chifu wa kabila Fulani au kuwa kiongozi !!
Njia ambayo alifaa kufuata ndiposa afike pale ilibidi aende juu ya mlima na mabonde.Lakini Mugu alikuwa pamoja naye.Je haya yanaeleza kuhusu maisha yako?Mungu aishie anampango kwa ajili ya maisha yako!!
Anataka kuwa na wewe ili aweza kuinuwa.Kwa wakati mwingine umewahi kuwa na ndoto kwa ajili ya maisha yako na tumaini lako linaonekana limedidimia. Pia kwa wakati moja umekuwa na lengo fulani katika mawazo yako,lakini kwa kunga'ng'ana maishani umewacha lengo lako.Pengine umeshushwa moyo na kuwa na huzuni kwa sababu ya ndoto yako au ile ndoto yako kubwa imefungwa au jinsi ilivyokuwa na Yusufu ,umewekwa kando na watu wengine, au kurushwa katika kisima cha taabu ,mateso au,wamenena uongo juu yako.Tafadhali usisahau kwamba Mungu yuko na wewe!kuinuliwa kwako hakutoki kwa mwanadamu lakini kunatoka kwa Mungu!!
Haijalishi uko katika shida gani au shida yako ni kubwa kiasi gani au kutokuwa na tumaini katika hali zako.Mungu anaweza na anataka kuinuwa. Mungu anampango mzuri kwa ajili ya maisha yako ya usoni.Na hata iwapo watu wamekusahau,Mungu anakuona.Anakujua na hajakusahau usitaajabike maana Mungu hajakusahau mngojee Mungu naye atakubariki kwa wakati wake mweneyewe.
Wakati unakuja ,Mungu atakupa zaidi ya yale uliotarajia kupokea, kile unachostahili kufanya ni kutenda yale ambayo Bibilia inaeleza katika kitabu cha Yakobo 4:10 "Jidhilini mbele za Bwana naye atawaguza.Ambapo inamaanisha kusema:Kutenda vile anavyosema.Soma Bibilia amini bibilia na ufanye jinsi inavyosema.Usitarajie kuinuliwa kwako kutoka kwa mwanadamu lakini kutoka kwa Mungu.Hata iwapo itakwelekeza katika bonde:Baki kuwa mfuasi wa Yesu Kristo mwana wa Mungu aishie milele,atakuinua.Anaweza kubadilisha hali zako kwa wakati mfupi.
Na kwa sasa nitakuombea:Ewe Baba Mungu wangu.Naja kwako katika jina la Yesu Kristo kwa ajili ya huyu msikilizaji ambaye angepende kubarikiwa na kuinuliwa na wewe.Hatuhitaji kuwa na shauku lakini kuamini mambo yote yanawezekana .Kwa hivyo ninakuomba,Kwa wakati huu,kuokoa,kukomboa,kuweka uhuru na nguvu za uponyaji ziweze kuwafikia wasikilizaji na mtumishi wako.Ukawape usitawi kuinuliwa kwa hao wote ambao ni wafuasi wa Yesu Kristo.Tunakushukuru kwa ajili ya mambo yote ambayo unaenda kutenda katika maisha yao.Amina!

Translation of the promotion that God offers by: Alfred Musungu*************
NI NINI SENTENSI YA MAISHA YAKO.
Mahubiri na: Mwinjilisti Sieberen Voordewind.

Wandungu wapendwa ,wadada na marafiki.Ni jambo la kufurahisha kuwa katika mkutano huu katika jina la Yesu Kristo.Jina ambalo liko juu ya majina mengine yote.Kama mnavyoweza kuona nimechukuwa ua lililonyauka .Pengine utashangaa kwa nini nimefanya hivyo,sawa?Kwa sababu ni vyema kusema hii inaptikana katika mahali pa kutupa takataka kule nyumbani lakini siyo kwa madhibau mazuri sana.Kila mtu anajua kwamba hii ilikuwa mbegu ndogo sana lakini ilikuja ikawa ya maana na ya kupendeza sana.Hatuwezi kueleza sana,maana ilianguka na kufa.Na hivyo ndivyo ilivyo na maisha ya mwanadamu, na yangu.Kuna wakati wa kuingia na kutoka .Maisha siyo mafupi.Mungu alituahidi kuishi maisha ya miaka sabini(70)na kwa wale ambao wana nguvu waishi miaka themanini (80) .Lakini kuna watu ambao wanaishi miaka zaidi ya mia moja.
Ujumbe ambao ninakuletea nikiwa na rehema unaitwa :Ni nini sentensi ya maisha .Na tukatazame neno la ajabu la Mungu katika kitabu cha Yohana 1:1-12 ni kifungu kinachojulikana lakini ni cha muhimu sana.

Mstari wa kwanza unaeleza :Hapo mwanzo kulikuweko Neno,naye neno alikuweko kwa Mungu ,naye Neno alikuwa Mungu."

Kuwa Mtulivu:Neno la neno liko katika kiyunani (Greek)Logos!Logos humaanisha sentensi muhimu kusudio,kuzaa matunda au sentensi muhimu .Tunaweza pia kusoma kulingana na Rev.D. Voordewind:"Hapo mwanzo kulikuwa na matarajio na haya yalikuwa na Mungu na yakawa ya Kiungu."Sentensi inamaanisha nini au umuhimu wa sentensi ,inamaanisha tamanio maoni na hukumu .Lakini haya siyo ninayo maanisha .Au katika hali ya kuhudumu kuingine kunaweza kuwa bila sentensi .Kile ninacho maanisha ni NI NINI .Kwa nini ninaishi?umuhimu wa sentensi unahusisha kuishi sasa na siku za usoni.Maana ya usoni inaashiria maisha yako kwa wakati huu.Je unaona giza katika maisha yako ya usoni kuliko vile unavyoishi sasa.Je unaona maisha yako yamekosa maana kuliko vile unavyoishi katika giza.

Ninakupa mfano wa haya ni nayo sema, mfano ,msichana wa miaka kumi na nne ambae wazazi wake walichukua talaka naye akaona kuwa maisha yake ilikuwa ya shida na kufinyiliwa; shuleni alikutana na rafiki mbaya ambae alimuambia :Anajua jibu la shida zake Chukua marijuana.alianza pole pole na mwishowe ikakolea na kuwa dawa ya kulevya."Asilimia tisini na tano(95%) wamenaswa na madawa ya kulevya .Kule wilaya maelfu ya vijana wanatoroka nyumbani bila kurudi tena wengine wao wamenaswa na madawa ya kulevya.Wacha turejelee yule msichana .Siku moja alichukuwa dawa yenye nguvu sana LSD matokeo yake ni kwamba alifikiria kuwa anaweza kupaa au kuruka umbali wa mita kumi kuenda chini.Na maisha yake yaliishia katika sanduku ndogo chini ya mchanga .Kila mtu ambaye anaona maisha yake kuwa haina maana anatembea katika giza.I wapo hata pata usaidizi wowote mwishoe itakuwa ya huzuni sana.Niruhusu ni kuelezee hili jambo la kujaribu kujinyonga limeongezeka katika ulimwengu wote:haswa katika nchi ya Uholanzi.

Bila kutojali imekuwa kama janga kule Uropa .Sana kule Usuisi ,Hangari ambayo tunaongea juu yake ,wafanyi kazi wengi asili mia sitini (60%) wamekumbwa na shida hii.Kulingana na mhubiri D.Voorderwind(ambae anafunza kutoka kwa Frankl)

Vikto Frankl Daktari wa akili alitumia Therapi ya hali ya juu katika watu elfu kumi na mbili kwa muda wa miaka minne.katika kila hali aligundua kwamba watu wengi huona maisha yao kuwa ya shida na ya kufinyuliwa .

Huyu daktari wa akili Frankl aligunduwa kule Australia asili mia ishirini ya idadi ya watu ambao anahusika nao na wana shida asili mia tisini ni walevi wa pombe ambao huo maisha yao yamepotokwa na haina maana.Nahatujawahi hesabu wale ambao wamenaswa na madawa ya kulevya.Karibu nusu ya vijana huona maisha yao haina maana kabisa Idadi hii ni ishara katika ukuta .Je tutafanya nini?Tuache sida hii ikuwe kubwa au tufanye jambo Fulani uhusu hii shida.Je unapata jibu kwa wale ambao wanaona maisha yao kuwa ya shida na kufunguliwa ?usisahau, Unahitaji kupata jibu mwenyewe, kwa nini?

Je utawezaje kusaidia mtu iwapo haujapata jibu kwa ajili ya maisha yako, wewe mwenyewe kama hauna jibu kuhusu sentensi ya maisha kuliko kuchakuwa bila kuelewa.Dk Jung aligunduwa.Theluthi

ya wangojwa wanashida kuhusu sentensi ya maisha na kwa hivyo wamekuwa wafungwa wa mawazo na hawana akili Timamu na kama haujui maana ya haya maneno unaweza kuangalia polepole katika kamusi.Iwapo unafikiri maisha yako haina maana ,basi ungali unashida kubwa . "Mgonjwa ambaye amepoteza tumaini au ujasiri wa kuishi atakufa tu kutokana na homa ya kawaida .Bruno Betleheim alikuwa katika vita vya dunia vya pili baada ya kukatiswa kwa huduma katika kambi .Aligunduwa kwamba wengi wa wafungwa AMBAO WALIKUFA KWANZA hawakuwa imani na ujasiri kuhusu sentensi ya maisha .Ndio haya yote yanawezakuwa matokeo yake.Iwapo wewe ni mtu ambaye unashida kuhusu sentensi katika maisha yako unaweza kuona kwa wakati huu wakutilia mkazo KUJIFUNZA KWA NENO la ajabu la Mungu.

JE NI NINI SENTENSI YA MAISHA YAKO.

Iwapo ungependa kujuwa sentensi ya maisha yako,Ni lazima urudie chanzo cha sentensi muhimu ,yafaa tutambue ukweli kuhusu maana ya maisha .Ukweli kwa hakika hauwezi kupatikana katika ulimwengu huu.Unaweza kuishi kama mpumbavu katika ulimwengu huu.hata na tamaa, lakini ni kwa muda mfupi tu.Ni kujiburudisha kwa muda .Lazima maisha yako ikuwe ya maana au kuzaa matunda leo na hata milele.

Bibilia inasema katika Yohana 1:4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima,nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu."

Sentensi ya maana inahusika haswa na maisha.Una sentensi ya maana katika maisha, Mungu ndiye chanzo cha uzima ,Uzima wa milele .Yohana 3:16 ili kila mtu amuaminiye asipotee ,bali awe na uzima wa milele ."Mungu ndiye chanzo cha maisha na sentensi ya maana katika maisha.Tunasoma katika Yohana 1:1 uzima unatoka kwa Mungu.Kwa nini ?kwa sababu yeye ndiye chanzo cha uzima.Yeye ndiye aliyeumba watu,wewe na mimi.

Kwa mfano, usiku mmoja muhalifu alizurura katika mji akitafuta kazi na akapita kando ya gari letu na akasoma maandishi haya ; "Njoni kwangu ninyi nyote msumbukanao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha" Wakati huo alikuwa na shida ya sentensi ya maisha. Alikuja kututembelea na kupeana maisha yake kwa Yesu kristo.Ninafikiria kuhusu kahaba ambaye alisema kwamba hatakubali Yesu kristo katika maisha yake, lakini alikubali kristo kama mwokozi katika maisha yake ,lakini alikubali Kristo kama mwokozi katika maisha yake njioni moja. Kile ambacho hawa watu wawili walikuwa nacho katika maisha yao ni kwamba hawakuona sentensi ya maisha yao.

Kile ambacho tunajifunza kutokana na haya kuna sentensi ya kuishi sentensi ya maisha ni hii.

a) Umeumbwa kwa mfano wa Mungu ,umeumbwa kufurahia Uzima ,uumbaji ,uumbaji wote umegeuzwa kwa watu kuleta utukufu kwa jina la Mungu.

b) Kujifahamu mwenyewe wewe ni nani umeumbwa na Mungu na kujifunza uumabji.

c) Sentensi ya maisha ni hii kwamba wewe ,juu ya kujua muumbaji wako lakini siyo kujua tu.Hiyo ni kuwa umbali sana.Mungu angependa ukuwe na uhusiano wa karibu na yeye.Uhusiano wa kweli.Ya kwamba pia wewe umeumbwa na Mungu.

Katika shamba la Eden binadamu wa kwanza alikuwa na uhusiano na muumbaji wake.Uhusiano huu uliweza kuvunjwa na dhambi lakini sababu ya Yesu Kristo mwana wa Mungu alitufia dhambi zetu na deni wewe na mimi tuweze kufahamu uhusiano wetu tena.
NINAKUPA MFANO WA HAYA.

Baba na mtoto walishi katika hali ya kukosana kila mara.Wangegombana kila waklati mmoja baba alilazwa hospitalini akiwa mgonjwa mahututi .Mama aliamua kumuAndikia kijana yake barua akimuuliza kuja hospitali kuona baba yake.Kitambo tu kijana aliposimama kando ya kitanda,mama alishika mikono yao yote na kuunganisha wote .Kwa hivyo kugombana kwa muda mrefu kuhuliisha wakati huo.Kile ambacho mama alifanya ni kile ambacho Yesu alifanya pale Calvary kwa ajili yake na ya baba.Hapo aliponyosha mkono wake uliokuwa umechibuka kwako na kwangu na ulimwengu wote na baba.

Kwa kutoa dhabihu aliweza kulipa deni na kurejesha uhusiano.

Iwapo utakubali hii dhabihu maisha yako itakuwa kamilifu na ya maana.Hautaishi katika giza .Lakini katika mwangaza na kufurahia uzima.Kwa hivyo kile ambacho unaweza kujifunza kwa huu ujumbe uliyo na nguvu ni kwamba maisha bila uhusiano wako na muumba wako,Mungu wa mbinguni na dunia ,miasha yako haina maana profesa.W.Jury alieleza kwamba katika maisha isio na maana haina ukweli ndani mwake .Lakini kuna ukweli .Pia kuna maisha ambayo inastahili .Yesu kristo alisema kwetu sisi "MIMI NDIMI NJIA ,UKWELI NA UZIMA!"

Haya maneno tatu yanaunda maana ya sentensi muhimu :Ni uzima ,uzima katika uhuru ,uzima wa milele unaishi kufurahia maisha .Ukweli pengine unaweza kusema: "Ndugu Voordewind ukweli ni nini? Ukweli ni huu:Yule aliyezaliwa na bikira Maria ,alikufa kwa ajili ya dhambi na deni letu na akafufuka kutoka kifoni .Ni jambo la mwisho sentensi muhimu katika NJIA. iwapo utatembea kwa njia ambayo itakuelekeza kupata uzima na katika paradiso ya mbinguni kwa hivyo hakuna sababu ya kufanya ukuwe na wasiwasi na maisha ya usoni ambayo imo gizani lakini SABABU sote ni kwako KUISHI.

Iwapo wewe ni mtu anaye sema "Nimepokea jibu,kwa hivyo ni nini maana ya maisha yako.Lakini kukosa uhusiano na muumbaji ambaye ni Mungu .Nina kukaribisha usongee karibu na madhabau .Ningependa kusema :usiwe na mawazo iliyo tawanyika nifanye au nisifanye lakini fanya uamuzi sasa pia kwa wale watu ambao wameswa na madawa ya kulevya au wale ambao wamefungwa katika uovu Fulani dhambi au magonjwa mengine.Niko na habari njema kwa ajili yako.Pengne umefungwa na minyororo lakini ni nini ninakusikia kama hapo awali ,sauti ya minyororo ambazo zinavunjika ?Ni kama vile ninasikia sauti ya Yesu Kristo ambayo inasema: "Yote yamekwisha : "Amemaliza dhambi zako ,magonjwa na udhaifu juu ya msalaba pale Calvari .Alilipa gharama ili upate kuishi katika ushindi .Nikiwa na furaha ningependa kuomba kwa ajili ya haya mahitaji na kualika kusongea karibu na madhabau.

Sikiliza haya:Na usiwahi sahau Mungu ambaye anakupenda sana na amefanya kila mambo yote ambayo itakufanya uishi na makusudi Fulani na kuwa na sentensii ya maisha."Amina.

Ujumbe huu umetafsiriwa na mchungaji :Alfred musungu.

***************
Tafakari Radioni Na Maombi:Na
Mwinjilisti Sieberen Voordewind.
Radio Hoogeveen (Udachi)
Mtazamo wa 3 Aprili 2007
Mpendwa msikilizaji,Muda wa kipindi hiki Radioni,ninapenda kuongea juu
ya ujumbe wenye kichwa:
MSHAURI WAKO NI NANI?
Tafadhali fungua macho yako kwa ajili ya maneno yaliyo hai ya
Mungu,wakati unaposikiliza na pokea utajiri wa baraka.
Biblia inasema:"...na kila amwaminiye hatatahayarika." Warumi 9:33
Haidhuru una matatizo gani,Kwenye Biblia tunasoma habari za mtu ambaye
alipatwa na shida kubwa,jina lake ni Yehoshafati.
Biblia inasema yafuatayo katika 2Mambo ya nyakati 20:2-3a"Wakaja watu
waliomwabia Yehoshafati wakisema,wanakuja jamii kubwa juu yako watokao
shamu,toka ng'ambo ya bahari na tazama wako katika Hasasori-tamari (ndio
En-gedi). Yehoshafati akaogopa...."
(Swahili Union Version 1997)
Kama vile Yehoshafati,labda na wewe pia umepatwa na shida kubwa,au
umeishi kwa hofu,hofu kwa ajili ya siku za usoni,hofu ya kuachwa,hofu ya
kufa,hofu ya kupungukiwa;
Labda unaogopa kwamba hutapata upenyo wa kutokea kwenye shida.
Chochote unachohitaji an chochote unachoogopa,Swali ni hili:"Mshauri
wako ni nani?"
Ndiyo,unamwendea nani kwa ajili ya shida zako pamoja na hofu zako?:Fanya
kama Yehoshafati alivyofanya!Biblia inasema:"Yehoshafati
akaogopa,akauelekeza uso wake amtafute BWANA..." (Swahili Union Version
1997)
Aliamua kumtafuta BWANA kwa ajili ya mahitaji yake.Mungu asikiaye maombi
na kujibu yote kulingana na mapenzi yake makamilifu kwa majira yake.
Biblia inasema katika mstari wa 3-4 "Yeye Yehoshafati...akatangaza mbiu
ya watu kufunga katika Yuda yote.Yuda wakakusanyika pamoja ili wamtafute
BWANA."
Bwana asifie! Yehoshafati alipata kimbilio si kwa mwanadamu bali kwa
Mungu.Shida yake haikuhitaji tegemeo la kibinadamu,kwa kuwa aliomba
hivi:
"...maana sisi hatuna uwezo juu ya jamii hii kubwa wanaotujia juu
yetu;..." Mstari 12
Pengine na wewe unahisi kushindwa kukabili hali zilizokuzonga.Tatizo
lako ni la kibinadamu:Huna tumaini,Huwezi kuona upenyo.
Na kama Yeoshafati,Alivyosema:"Hatujui tufanyeje" Lakini,
MSHAURI WAKO NI NANI?
Unamwendea nani akusaidie?
Yehoshafati alimwendea Mungu na akaomba:"...lakini macho yetu yatazama
kwako."Mstari wa 12
Hakutazama uasi bali alimtazama Mungu aliye hai kwa imani,ambaye kwake
kila kitu kinawezekana.
Alipokuwa anaomba,Biblia inasema (mstari wa 14) "Ndipo
Yahazieli...akajiliwa na Roho ya BWANA...akasema sikieni,Yuda wote nanyi
mkaao Yerusalemu na wewe mfalme Yehoshafati;BWANA awaambia hivi:Na wewe
pia unayesikiliza mahubiri haya Radioni)"
Usiogope wala kukata tamaa,kwa sababu ya jeshi hili kubwa,"kwani vita si
yenu bali ni ya Mungu."
"Hamtahitaji kupigana vita,jipangeni mkauone wokovu wa BWANA ulio pamoja
nanyi,enyi Yuda na Yerusalemu;msiogope,wala msifadhaike;kesho tokeni
juu yao.kwa kuwa BWANA yu pamoja nanyi." (mstari wa 17)
Ndiyo,Wakati yeye na wengine wakiomba,RohoMtakatifu alikuja na majibu.
Ni muujiza!Nasi pia tuan kitabu kilichovuviwa na Roho Mtakatifu,ndani ya
kitabu hiki majibu yote yameandikwa,kitabu hiki ni Biblia!
Katika Biblia Mungu anakuambia hivi:
"Niite nami nitakuitikia,nami nitakuonyesha mambo makubwa,magumu
usiyoyajua...tazama nitakuletea afya na kupona..." (Yeremia 33:3,6)
Ukimruhusu Mungu aliye hai kuwa Mshauri wa maisha yako,basi atasema nawe
kupitia maombi,Biblia au njia nyingine.
Msaada wa Mungu ni msaada bora!Ushauri wake ni ushauri bora;fanya kama
Yehoshafati alivyofanya,Na fanya uamuzi kutafuta ushauri kwa mshauri
mwema:
Na kama ilivyokuwa kwa Yehoshafati,Bwaba atasikia na kukujibu.
Baada ya Bwana kumjibu Yehoshafati tunasoma:" Yehoshafati akainama
kichwa kifulifuli;wakaanguka mbele za BWANA Yuda wote na wakaao
Yerusalemu,wakamsujudia BWANA." (2 Mambo ya nyakati 20:18)
Hata kabla ya shida kutatuliwa,Yehoshafati,aliuamini ushauri wa
Mungu,akainama na kumwabudu Mungu.
Mungu anaposema nasi kwa njia ya maombi au Biblia,hatupaswi kwanza kuona
jibu la shida kwa macho ya kibinadamu,kwanza tunapaswa kuamini majibu
na ushauri wa Mungu.
Yesu alisema:"Kwa sababu hiyo nawaambia,Yoyote myaombayo mkisali,aminini
ya kwamba mnayapokea nayo yatakuwa yenu." (Marko 11:24)
Amini kwamba Mungu amesikia maombi yako kabla hujaona na kuhisi
mabadiliko.Anza kumshukuru kwa muujiza.Na kama ilivyokuwa kwa
Yehoshafati,Mungu atajibu maombi yako sawa sawa na mapenzi yake kwa
wakati wake,wewe nawe pia utatoka kwenye vilindi vya matatizo,na utaweza
pia kutembea kama Yehoshafati kwa furaha na amani:
Hili tunaweza soma kwenye neno la Mungu:
"Kisha wakarudi kila mtu wa Yuda na Yerusalemu,na Yehoshafati mbele
yao,ili kuurudia Yerusalemu kwa furaha;kwa kuwa BWANA amewafurahisha juu
ya adui zao.Wakafika Yerusalemu wenye vinanda vinubi na mapanda kwenda
nyumbani kwa BWANA.Ikawa hofu ya Mungu juu ya falme zote za
nchi,waliposikia ya kuwa BWANA amepigana juu ya adui za Israeli.Basi
ukatulia ufalme wake Yehoshafati;kwa sababu Mungu wake alimstarehesha
pande zote." (20:27-30)
Bwana asifiwe!
Yale yote ambayo Mungu aliye hai alimfanyia Yehoshafati,anapenda
kukufanyia na wewe pia kwa Jina la Mwanawe Yesu wa Nazarethi ambaye
alikuja duniani kuwatakasa wenye dhambi.
Popote pale ulipo wakati huu,nyumbani,gerezani,popote pale:Na twende kwa
Imani mbele ya kiti cha enzi cha Mungu.
"Ee Mwenyezi Mungu na Baba.katika Jina La ajabu la Yesu Kristo ninakuja
mbele zako kwa ajili ya wale wote wenye mahitaji wanaosikiliza kipindi
hiki Radioni.Hatuna shaka bali tunaamini kwamba wewe ni mkuu kuliko
shida yoyote ile. Na kwa hiyo tunaomba:Sauti yako,Ukombozi wako,Uhuru
wako,na nguvu yako ya uponyaji,ije sasa kutoka kwako,Ponya
wagonjwa,Ondoa maumivu,Ondoa Vifungo,hofu na ulevi,Ondoa matatizo ya
kifedha,Leta majibu kwa mahitaji yote.
Ee Mungu wajie wasikilizaji wote wa mahubiri haya Radioni,kwa uwezo wa
kimungu na upako ili kupitia somo hili,maisha yao yabadilishwe.
Nakushukuru kwani kwa huruma yako utasikia maombi haya,wakati
wako.Nasifu na kuheshimu Jina Lako"
Na rafiki zangu: Pokea uponyaji,Uhuru,Majibu na pokea Upako wa nguvu
wa Roho wa Mungu katika Jina La Yesu!
Amini na mshukuru Mungu kwa Hayo!
Na kamwe usisahau,"MSHAURI WAKO NI NANI?"
Nakutakia utajiri na baraka za Mungu,kwa Jina tukufu la Yesu Kristo,Jina
kuu kuliko majina yote.Amina.

Translated by: Shanel***************************************

BOEKEN:

 
LEES MEER OP: BOEKEN

AANBEVOLEN:


ZOEKEN/SEARCH:

COPYRIGHT:

© Sieberen Voordewind
Alles op deze website is auteursrechtelijk beschermd! Niets van deze website mag worden verveelvoudigd en/of openbaar gemaakt worden door middel van druk, fotokopie, microfilm, of op welke wijze dan ook, zonder voorafgaande schriftelijke toestemming van de auteur. All rights reserved. Exodus 20:15 / Jeremia 23:30 / Romeinen 2:21. DE AUTEURSWET IS VAN TOEPASSING OP ALLES WAT OP DEZE WEBSITE STAAT. Voor de link naar de wet klik op: AUTEURSWET